Loading

Shughuli za afya na matibabu katika kaunti ya Taita Taveta zasitishwa baada ya madaktari na wahudumu wote wa afya katika kaunti hiyo kuingia kwenye mgomo kulalamikia kutotimizwa kwa matakwa yao.

Wahudumu hao, waliokuwa wamepeana ilani ya siku ishirini na moja kwa serikali ya kaunti waapa kutorudi kazini hadi maslahi yao yashughulikiwe.

Mgomo huo, ambao umeingia siku ya pili leo umewaacha wanaohitaji huduma za kiafya kwenye hali tete na kulazimika kwenda kutafuta matibabu kwenye hosipitali za kibinafsi.

Wahudumu hao ambao wamelalamikia kucheleweshwa kwa mishahara yao kwa miezi kadhaa Sasa, wanadai kuwa hali hiyo imewafanya washindwe kukimu mahitaji yao ya kimsingi, ikiwemo kulipia watoto wao ada ya shule na mahitaji mengine.

Pia wamelalamikia ukosefu wa bima ya afya tangu Januari mwaka huu, hali ambayo imewalazimu kutumia akiba zao au kuchukua mikopo wanapougua.

Wakiongea na wanahabari walipokuwa wakifanya maandamano ya amani mjini Mwatate, madaktari hao wamesema kuwa hawatalegeza kamba hadi pale ambapo serikali ya kaunti itashughulikia malalamishi yao.

Erick Mrefu, mwakilishi wa maafisa wa kliniki amesema kuwa ukosefu wa vifaa vya kufanyia kazi unaeka maisha yao na wagonjwa hatarini.

“Hospitali sai hazina glavu, tunatumia glavu moja ambayo kisheria haifai,” Mrefu alisema.

Erick Mrefu pia alilalamikia ukosefu wa dawa kwenye hosipitali, Hali ambayo kulingana na yeye inavunja moyo kuona wagonjwa wakirudi manyumbani bila msaada unaofaa.

“Ukosefu wa dawa katika hospitali zetu inakwenda kinyume na taratibu za afya, ambazo zinalenga kuhakikisha kila mgonjwa anapata matibabu bora,” Mrefu alieeleza.

Richard Nyambu, muuguzi katika hosipitali ya rufaa ya Moi, ameeleza malalamiko yake kuhusu tatizo la makato ya mshahara yanayofanywa na mwajiri kwenda kwa taasisi za tatu (third party), ambazo zinasema hazipokei fedha hizo.

“Inasikitisha kuona mishahara yetu inapokatwa, lakini bado tunaendelea kupata malalamishi kutoka kwa hizo taasisi kwamba hazijapokea michango yetu,” Nyambu alilalamika.

Nyambu aliendelea kusisitiza kuwa ukosefu wa uwazi na ufanisi katika usimamizi wa makato hayo unawaeeka wafanyakazi katika Hali ya wasiwasi na vile vile kukiuka taratibu za ajira na haki zao.

Chama cha madaktari Kenya (KMPDU) wapeana ilani ya siku kumi na nne kwa serikali za kaunti zote kuhakikisha kuwa wanatimiza matakwa ya wanachama hao na iwapo serikali za kaunti zimeshindwa kukimu mahitaji yao basi warudishwe chini ya usimamamizi wa serikali ya kitaifa.

View all posts

By root

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp