Loading

Mwakilishi wa wanawake kwenye kaunti ya Taita Taveta Lydia Haika aongoza Hafla ya zoezi la usambazaji wa Sodo kwa Wanafunzi wa Shule za umma kwenye Maeneo Bunge ya Mwatate, Voi, Wundanyi na Taveta mtawalia.

Shule 217 zimelengwa kufikiwa na mpango huo wa Sodo kwa Wanafunzi ambapo Serikali imeweka mikakati ya Kuboresha Mazingira ya Elimu ya Mtoto wa Kike kwa kuhakikisha Usambazaji wa Sodo kwa wanafunzi wenye kipato cha chini katika shue za umma kote nchini, Mpango Ulioshinikizwa na Serikali kuu kwa Ushirikiano na Wawakilishi wa wanawake kwenye Kaunti zote Arobaini na Saba.

Wanafunzi Elfu Kumi na Tano Mia Nne themanini na tisa (15, 489) katika Shule Mia Mbili na Kumi na Saba (217) kwenye kaunti ya Taita Taveta wameweza kunufaika na Sodo huku wengine wakipata Ufadhili wa Basari ya Shilingi Milioni Mbili na Elfu Mia Nne (2,400,000).

“Wakati mlituchagua kwa kipindi cha pili, mimi niliongoza wenzangu kina mama tukaenda kwa Rais tukamwambia huu mpango wa sodo tunataka kuufanya kama wa mama kwasababu tuna uchungu wa wasichana tumeshapitia hapo na tutafanya kazi hii kwa bidii, ilikua mvutano hapa na pale lakini tunamshukuru Rais William Ruto kwani aliona nuru ndani yake na akakubaliana nasi tuweze kuendesha zoezi hili kama wawakilishi wakike katika kaunti zote nchini,” Haika alisema.

Kadhalika, wanafunzi hao baadhi yao wakiandamana na wazazi na walimu wao vilevile walipata fursa ya kuhamasishwa katika maswala kadha ya jinsi ya kujitunza kama msichana na vilevile jinsi ya kujinufaisha na Elimu na kuboresha Kamishina wa Kaunti ya Taita Taveta Bi. Josphine Onunga, Mkurugenzi wa Elimu eneo bunge la Mwatate Dorothy Wamboi Karago miongoni mwa wengine wakiwemo walimu wakuu wa shule na wafanyikazi katika idara mbalimbali za serikali ikiwemo afisi ile ya Watoto.

“Watoto wetu wasichana wetu hamna sababu ila tu kuweka bidii kwa shule, muweke malengo na myafanyie kazi vilivyo ili kuyafikia,” alisema Onunga.

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Taita Taveta Lydia Haika akiongoza usambazaji wa sodo kwa wanafunzi. Picha| Julius Mariki.

“Langu nikuwahakikishia kwamba serikali imejitolea kikamilifu na lazima tuhakikishe kwamba watoto wote wakisichana wako shuleni, na kwa wasichana serikali iko nanyi iwapo uko na jambo lolote linakusumbua kimbia kwa mwalimu ama uje kwetu utuambie tutakusaidia lakini usikubali kudanganywa na vijana na wanaume kule nje, msibabaishwe na msipotoshwe bali zingatia masomo na elimu yako ili ufanikiwe maishani,” Onunga aliongeza.

“Shule zetu hapa mwatate zinafanya vizuri hata wakati wa mgomo wa walimu wa kuppet shule zetu zilikua imara na walimu wetu wa BOM waliweza kutushikilia vizuri. Nashukuru kwa mpango huu wa sodo kwani hili litaweka mtoto wa kike shuleni, zama zile zimepitwa na wakati ambapo wanafunzi watakosa shule sababu ya hedhi.” Mkurugenzi wa elimu Dorothy Wamboi alisema.

Wakati uo huo wito zaidi ulitolewa kwa wazazi kuzingatia elimu ya wanao hasa katika kuwapatia uwezo wa kuafikia malengo yao kielimu na maono ya kuimarisha Maisha yao ya badaye.

Swala la Mtoto wa kiume liliibuka wito ukitolewa kwa mwakilishi huyo Lydia Haika kumjumuisha mtoto wa kiume katika mipango ya kuimarisha elimu ya mtoto huyo wakiume na kumuwezesha katika kuboresha Maisha yake ya badaye.

Haika aitha alikubaliana na wito huo akiahidi kuhusika katika kuweka mikakati ya kuboresha hali za mtoto wakiume akiwa shuleni miongoni mwa maswala mengine mhimu ikiwemo kuwapa hamasa wanapo balehe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp