![]()
Kwa muda mrefu ukulima umefeli, wakulima wamepata hasara, baada ya misimu ya
mvua kubadilika, kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Japo changamoto kama ugonjwa wa honeydew, leaf blight, mvua nyingi na ushindani
kutoka kampuni za nailoni, zao la mkonge limedhihirika kuwa hakika, haswa katika
sehemu kame na nusu kame nchini.
Data kutoka halmashauri ya Agriculture Food Authority, AFA, inasema mkonge hutoa
asilimia 90 ya mazao na inafanya vyema sehemu za Kilifi, Makueni, Mogotiyo kaunti ya
Baringo, nakuru, siaya, migori na kaunti ya Taita Taveta.
wakulima wamedhihirisha furaha yao kwa ukulima wa mkonge mbali na vyakula asili,
haswa wakati huu ulimwengu unakabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Je jawabu ni lipi kwa wakulima haswa baada ya kubadilika kwa misimu ya mvua?
Sikiliza makala maalum iliyotayarishwa na mwandishi wetu Lina Mwamachi. Bofya kiungo kilicho hapa chini ili kusikiliza.