![]()
Viongozi wa usalama kaunti ya Taita Taveta wamelaumiwa kwa kudorora kwa usalama wa waendeshaji piki piki katika kaunti hiyo huku wito ukitolewa kwa idara husika kuwajibika.
Kulingana na mbunge mteule katika jimbo la Taita Taveta Mohamed Dudu visa vya boda boda kuvamiwa na wahuni na kupigwa na kujeruhiwa na pia kuibiwa piki piki zao vimekithiri Taita Taveta huku kisa cha karibuni ikiwa vijana wawili wa boda boda waliodungwa visu na kujeruhiwa vibaya kabla ya piki piki zao kuibwa.
“Ni jambo la kusikitisha kuona vijana wetu wawili wa boda boda juzi tu walivamiwa na kudungwa visu na wahuni ambao baada ya kuwashika na kuwapeana kwa askarai waliachiliwa huru licha ya madhara waliofanyia wendesjaji piki piki wetu” asema Mohamed Dudu.
Katika ujumbe wake kwa viongozi wa Taita Taveta Dudu amemuuliza mwakilishi wa kina mama kaunti hiyo Lydia Haika kushirikiana na viongozi wengine katika kaunti hiyo kushinikiza vitengo vya usalama kuwajibikia usalama wa jamii yote.