![]()
Mwakilishi wa kike katika kaunti ya Taita Taveta Bi. Lydia Haika ambaye yuko na amza ya kuwania nafasi ya useneta wa kaunti hiyo katika uchaguzi ujao amepigwa jeki kisiasa baada ya wawakilishi wadi katika bunge la Taita Taveta kutangaza kumuunga mkono katika safari yake ya kisiasa.
Lydia Haika ambaye alichaguliwa mwaka 2017 kama mwakilishi wa kina mama jimbo hilo kupitia chama cha KENYA KWANZA amesalia imara katika siasa zake licha ya eneo hilo kutajwa kuwa ngome ya upinzani na kuchaguliwa kwa awamu mbili.
Wawakilishi wadi hao wakiongozwa na Dorcas Mlughu wa wadi wa Rong’e, Newton Kifuso wa Wumingu Kishushe, Lilian Kidali na Mohamed Dudu wawakilishi wateule wamemtaja Lydia Haika kama kipenzi cha wengi na kiongozi mwenye sikio la mwananchi.
https://web.facebook.com/reel/878049872041503
“Jameni wakaazi wa taita taveta hasa nyinyi kina mama jinsi mulivyomchezea mama Haika hapa kwa upendo isiwe ni kucheza tu hapa lakini pia muonyeshe upendo wenu zaidi katika uchaguzi ujao kwa kumpigia kura kama seneta wa kwanza mwanamke Taita Taveta” kauli ya Mohamed Dudu
Naye mwakilishi wa Kishushe Newton Kifuso pia aliongeza sauti yake kwa kumtafutia mama Lydia Haika kura za useneta kwa wananachi wa Voi.
“Tunavyomjua mama Haika amekua na juhudi za kuwasaidia vikundi vya wamama, vijana na walemavu na pia katika uongozi wake ameonyesha nia ya kutoa suluhishwa kwa matatizo ya wananchi. Hivyo basi kama alivyosema Dudu hapa tumeona mumemchezea sasa Haika kwa furaha ya yale amewafanyia basi sasa mumuonyeshe upendo huo kwa kumpigia kura” asema Newton Kifuso.
https://web.facebook.com/reel/1711421083195821
Mwakilishiwa Rong’e ambaye alichaguliwa kwa chama cha UDA Taita taveta na mwakilishi wa kike pekee aliyechaguliwa alimtaja Haika kama kiongozi mkakamavu na mwenye hemka ya kukutansha viongozi wengine katika maendeleo akisema utendaji kazi wake unaonekana dhahiri katika kila pembe za jimbo la Taita Taveta.
“Katika kaunti hii ya Taita Taveta mimi namtambua sana mama Lydia Haika na aliyekua mbunge wa Taveta Naomi Shaban kama wanawake shupavu sana katika siasa ukanda wa pwani. Viongozi hawa wamenishika mkono sana katika saisa zangu kama mwanamke na nimefaulu, vivo hivyo ifikapo mwakani uchaguzi wa 2027 nitajitahidi sana kumsaidia mama Lydia Haika amekua seneta wa kwanza mwanamke taita taveta’ asema Dorcus Mlughu.
Kauli hizi zinashamiri licha ya mchuano wa mchujo katika nafasi hio hio ya useneta katika chama tawala cha UDA Taita Taveta ambapo kwa sasa nafasi hiyo imewavutia viongozi kadhaa wakiwemo aliyekua gavana wa kwanza Eng. John Mrutu, aliyekua mwakilishi wadi wa Saghala Godwin Kilele na mama Lydia Haika miongoni mwa wengine.
Kwa sasa wakaazi wa taita taveta watasubiriwa endapo uchaguzi ujao wa mwaka 2027 watavunja minyororo ya kuchagua viongozi kwa jinsia ama watazingatia sera za kiongozi.